Tuesday, March 6, 2018

AGPAHI YAOMBWA KUSAIDIA DAWA ZA MAGONJWA NYEMELEZI KWA WATU WENYE VVU WILAYANI BUKOMBE

Kaimu Mganga Mkuu wa Halmashauri ya Wilaya ya Bukombe Mkoani Geita Irene Mukelebe, akiongea na waadishi wa habari Ofisi kwake  wakati Timu ya waandishi wa habari pamoja na watalaamu kutoka AGPAHI waliotembelea kituo hicho kujionea huduma zinavyotolewa kwa watu wanaoishi na Virusi vya Ukimwi.

Kaimu Mganga Mkuu wa Halmashauri ya Wilaya ya Bukombe Mkoani Geita Irene Mukelebe, akielezea namna ambavyo wameweza kupata manufaa kutokana na ufadhili ambao umekuwa ukitolewa na shirikala la Ariel Glaser Pediatric AIDS  Healthcare Initiative (AGPAHI) Wilayani humo.  

Uboa  ambao unaelekeza huduma za afya zinazotolewa kwenye zahanati ya Bugelenga.

Zahanati ya Bugelenga .

Kaimu Mganga Mfawidhi Zahanati ya Bugelenga iliyoko Wilayani Bukombe Mkoani Geita Hawa Mussa, akionesha chumba cha sindano kwenye zahanati hiyo.

Kaimu Mganga Mfawidhi Zahanati ya Bugelenga iliyoko Wilayani Bukombe Mkoani Geita Hawa Mussa, akiongea na waandishi wa habari pamoja na watalaamu kutoka AGPAHI waliotembelea kituo hicho kujionea huduma zinavyotolewa kwa watu wanaoishi na Virusi vya Ukimwi.

Kaimu Mganga Mfawidhi Zahanati ya Bugelenga  Hawa Mussa, akiwa nje ya jengo la zahanati hiyo na na waandishi wa habari pamoja na watalaamu kutoka AGPAHI waliotembelea kituo hicho kwa lengo la kujionea namna ambavyo  huduma zinatolewa kwa watu wanaoishi na Virusi vya Ukimwi.

Afisa Mradi wa Tiba na Matunzo unaojulikana kama  Boresha unaotekelezwa na AGPAHI mkoa wa Geita  Bw,Adam Masesa  kiongea na waandishi wa habari juu ya utekelezaji wa mradi huo katika mkoa wa Geita.

Halmashauri  ya Bukombe mkoani Geita inakabiliwa na changamoto ya ukosefu wa dawa za magonjwa nyemelezi kwa watu ambao wanaishi na Virusi vya UKIMWI(VVU).

Kutokana na tatizo hilo Kaimu mganga mkuu wa halmashauri  hiyo,Irene Mukebe,ameliomba shirika ambalo sio la kuserikali la Ariel Glaser Pediatric AIDS  Healthcare Initiative (AGPAHI), kutoa msaada wa dawa hizo ambazo zitasaidia kuendeleza mapambano ya maambukizi ya virusi vya Ukimwi.

Dkt  Mukelebe, alisema  kuwa upatikanaji wa dawa hizo umekuwa mgumu kutokana na kukosekana katika bohari ya Dawa (MSD) ambayo imekuwa ni tegemeo kwenye halmashauri hiyo .Na kwamba tatizo jingine ni dawa hizo kuwa na gharama kubwa katika kuzinunua,  huku wagonjwa wengi ambao wanaishi na maambukizi kutokuwa na uwezo wa kumudu gharama za manunuzi.

Alisema kuwa uwezo wa halmashauri kuweza kumudu gharama za dawa hizo umekuwa mdogo kila mwaka, kutokana na mahitaji kuwa makubwa kwa halmashauri mzima, ambapo aliomba msaada kutoka AGPAHI kutatua changamoto hiyo.
" Ombi letu kubwa kwa AGPAHI licha ya kutusaidia sana katika kuwahudumia watu wanaoishi na Virusi Vya UKIMWI, watusaidie kupatikana kwa dawa hizi maana mahitaji ni makubwa sana" alisema Mukelebe.

Aliongeza kuwa katika halmashauri hiyo kiwango cha maambukizi ni asilimia 5, ambapo watu wengi wanaoishi na Virusi Vya UKIMWI katika halmashaur hiyo wamekuwa wakikabiliwa na magonjwa nyemelezi ukiwemo Ugonjwa wa Mkanda wa jeshi, TB pamoja na Fangasi.Na kwamba  wagonjwa wengi ambao wamekuwa wakiacha kutumia dawa za kufubaza Virusi Vya UKIMWI (ARV) wamekuwa katika hatari zaidi ya kupoteza maisha kutokana na kushambuliwa kwa kasi na magonjwa hayo.

Pia amegusia utekelezaji wa   Mradi wa Tiba na Matunzo unaojulikana kama  Boresha unaotekelezwa na AGPAHI, kwenye Halmashauri hiyo alisema kuwa shirika hilo limesaidia kwa kiwango kikubwa kuboresha huduma kwa watu wanaoishi na Virusi vya Ukimwi.

alifafanua  kuwa Shirika hilo limesaidia kuboresha huduma za wagonjwa hao katika maeneo ya kutolea huduma za Afya kitengo cha Tiba na Matunzo (CTC) kwenye vituo vya Afya na Zahanati 5 ikiwa pamoja na kutoa mafunzo kwa wataalamu wa afya jinsi ya kuwahudumia wagonjwa hao.

Kutokana na  Ombi hilo Afisa Mradi kutoka AGPAHI mkoa wa Geita Adam Masesa alisema kuwa kwa sasa shirika hilo linatekeleza Mradi wa Tiba na Matunzo unaojulikana kama  Boresha ambapo alisema lengo lake siyo kununua dawa.

Masesa alieleza kuwa kupitia mradi huo shirika limejikita sana katika kuboresha huduma kwa watu wanaoishi na Virusi vya Ukimwi, kwa kuboresha vitengo vya Tiba na Matunzo CTC, kusaidia katika upatikanaji haraka wa vipimo kwa wagonjwa hao, pamoja na kutoa mafunzo kwa watalamu wanaowahudumia watu wenye VVU.

" Kama Afisa Mradi tumelipokea ombi la Halmashauri ya Bukombe na nitalifikisha kwa wahusika, lakini katika mradi huu kipengele cha kutoa dawa hizo hakipo na badala yake tunaboresha huduma sehemu wanapopata matibabu yao" Alisema Adam.

Aidha waandishi wa habari pamoja na afisa kutoka AGPAHI na Afisa habari wa Mkoa wa Geita wameweza kutembelea Zahanati ya Bugelenga na kufanikiwa kuzungumza na kaimu mganga Mfawidhi wa zahabati hiyo,Hwa Musaa ambapo alisema kuwa zahanati hiyo inakabiliwa na dawa hizo kwa wagonjwa wanaoishi na Virusi Vya Ukimwi.

na kwamba wameendelea na jitihada za mala kwa mala za kuomba kwa wahisani pamoja na serikali  lakini wamekuwa wakijibiwa kuwa dawa kwa sasa hazipatikani na wakati mwingine zimekuwa zikija  chache kuliko mahitaji halisi.